AfCFTA kuhimiza matumizi ya sarafu za kienyeji ili kupiga jeki biashara ya kikanda
2022-06-15 08:42:23| CRI

Eneo la biashara huria la Afrika (AfCFTA) limesema litahimiza matumizi ya sarafu za kienyeji ili kupiga jeki biashara miongoni mwa nchi za Afrika.

Mshauri mkuu wa kiufundi wa eneo hilo Bw. Prudence Sebahizi amewaambia wanahabari mjini Nairobi kuwa kwa sasa sehemu kubwa ya biashara ya ndani ya Afrika inafanyika kwa dola ya kimarekani.

Amesema matumizi ya sarafu za kienyeji yataongeza miamala na kupunguza muda unaotumika kufanya malipo, na hivyo kuhimiza biashara miongoni mwa nchi za Afrika.

Bw. Sebahizi amesema eneo la biashara huria la Afrika linashirikiana na Benki ya Exim ya Afrika kuanzisha mfumo wa malipo kwa nchi za Afrika kwa kutumia sarafu za ndani kwenye biashara ya ndani ya Afrika.