Baraza la biashara la Afrika Mashariki lasaini makubaliano na Taasisi ya utafiti ya Afrika ili kuongeza ushindani
2022-06-16 10:01:33| CRI


Baraza la biashara la Jumuiya ya Afrika Mashariki EABC, ambalo ni chombo kikuu cha kikanda cha sekta binafsi limesaini makubaliano na Taasisi ya Utafiti wa Elimu ya Juu ya Afrika AHERI, ili kuongeza ushindani wa kikanda.

Mkurugenzi mtendaji mkuu wa Baraza hilo Bw. John Bosco Kalisa amesema mjini Nairobi kuwa makubaliano hayo yanatoa mpango wa ushiriki katika miradi ya utafiti ya pamoja ambayo itaboresha uvumbuzi wa bidhaa na huduma mpya katika eneo la Afrika Mashariki zitakazokidhi mahitaji ya masoko ya bara na kimataifa.

Bw. Kalisa amesema kupitia ushirikiano huo, watatetea utungaji wa sheria kuhusu hakimiliki ya ujuzi na kutatua tatizo la kutolingana kwa ujuzi, ili kuimarisha ushirikiano kati ya sekta ya taaluma na sekta ya viwanda katika Afrika Mashariki.

Pia ameeleza kuwa ushirikiano unaamuliwa na uvumbuzi wa bidhaa ambao utaimarisha uwezo wa uzalishaji na ushindani wa biashara ya kikanda.