Maandamano ya amani yafanyika Kaskazini Mashariki kwa DRC kupinga kundi la M23
2022-06-16 08:49:24| CRI

Maandamano ya amani yamefanyika mji wa Goma katika Jimbo la Kivu Kaskazini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo kupinga mashambulizi yaliyoanza kufanywa hivi karibuni na kundi la M23, ambalo siku chache zilizopita lilitwaa udhibiti wa mji wa Bunagana.

Jana jumuiya za kiraia na makundi ya harakati za vijana yaliandaa maandamano hayo kupinga kundi la M23 kutwaa mji wa Bunagana, ambao ni kituo muhimu cha kivuko kati ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo na Uganda. Waasi wa kundi hilo pia waliwahi kutwaa mji huo mwaka 2012.

Mamlaka za Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo zimekuwa zikiilaumu Rwanda kwa kuliunga mkono kundi la M23, Rwanda imekuwa inakanusha shutuma hizo na kulilaumu jeshi la Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo kwa kushirikiana na waasi wa Rwanda wa kundi la FDLR walioko mashariki mwaka nchini hiyo, ambalo baadhi ya watu wake wanalaumiwa kuhusika na mauaji ya kimbari ya mwaka 1994.