Wanasayansi wa Uganda wajenga mfumo wa gharama ya chini wa kusimamia ubora wa hewa
2022-06-16 08:48:49| CRI

Wanasayansi 15 vijana katika Chuo Kikuu Cha Makerere cha Uganda wamejenga mfumo wa gharama ya chini wa kusimamia ubora wa hewa, ambao wataalam wanasema utakuwa na ushawishi katika kufanya maamuzi ya kukabiliana na ongezeko la uchafuzi wa hewa nchini humo.

Wataalamu wanasema mfumo huo utaweza kusaidia kufanya maamuzi ya wakati huo huo, na kuchangia kwenye kufanya maamuzi kwenye ngazi ya mtu mmoja, kata na hata taifa, kuhusu sera za kufuata kupunguza uchafuzi wa hewa.

Kwa mujibu wa takwimu za mwaka 2021 kuhusu ubora wa hewa duniani, mji wa Kampala ulitajwa kuwa moja ya miji yenye uchafuzi zaidi duniani ، viwango vyake vikiwa ni zaidi ya mara 5 hadi 7 ya ukomo wa viwango vya S shirika la afya duniani WHO.