Wataalam wa matibabu wa Sudan Kusini wapata ujuzi wa upasuaji kutoka kwa wenzao wachina
2022-06-17 08:42:31| CRI

Madaktari wa Sudan Kusini kwa mara ya kwanza wamejifunza ujuzi wa kimsingi kutoka kwa wenzao wachina kufanya upasuaji mkubwa, hasa upasuaji wa laparoscipic.

Mafunzo hayo yalitolewa jana na daktari mkuu wa kikundi cha tisa cha madaktari wa China Ding Zhen, kwenye hospitali ya mafunzo ya Juba.

Mkuu wa idara ya uzazi na magonjwa ya wanawake wa hospitali hiyo Bw. Moses Maror, amesema mafunzo hayo yameboresha ujuzi wa madaktari 20 ambao kabla ya hapo hawakuwa na ujuzi kuhusu upasuaji wa namna hiyo.

Amesema ushirikiano kama huo na wataalam wa China uliwasaidia kufanya upasuaji wenye mafanikio mwaka 2018. Amesema zamani walikuwa na uwezo wa kufanya upasuaji mdogo tu, na upasuaji waliofundishwa na madaktari wa China walikuwa wakiusoma kwenye vitabu tu.