Wafanyabiashara wa Kenya watarajia kuongeza mauzo kwenye soko la China
2022-06-17 08:31:12| CRI

Wafanyabiashara wa Kenya wanatarajia kupanua biashara yao kwenye soko la China, ili kuongeza mapato.

Ofisa mkuu mtendaji wa Bodi ya Biashara na Viwanda (KNCCI) katika kaunti ya Nairobi Bw. James Odongo, amewaambia wanahabari kuwa baadhi ya bidhaa za Kenya zinazoweza kuuzwa zaidi nje ya nchi ili kukidhi mahitaji ya kimataifa yanayoongezeka ni pamoja na maboga, chai, maua na kahawa.

Akiongea kwenye jukwaa moja kuhusu biashara na uwekezaji lililofanyika Nairobi kwa lengo la kuhimiza mjadala kuhusu namna ya kuingia kwenye soko la China, Bw. Odongo amesema kuwa uhusiano wa kibiashara kati ya Kenya na China pia unatoa fursa ya kuhamisha ufundi na teknolojia kutoka China kwenda kwenye soko la ndani wakati Kenya inatafuta kuondokana na athari za janga la Covid-19.

Takwimu za serikali zinaonesha kuwa mwaka 2021, Kenya iliuza bidhaa zenye thamani ya dola za kimarekani milioni 186 kwenye soko la China.