Kenya na UNDP kuzindua kampeni ya amani kufuatia uchaguzi mkuu
2022-06-20 10:09:38| CRI

Kenya na Shirika la Mpango wa Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) Jumamosi walizindua kampeni ya amani ili kukabiliana na vurugu za uchaguzi kufuatia uchaguzi mkuu uliopangwa kufanyika Agosti 9.

Mandisa Mashalogu, kaimu mwakilishi mkazi wa UNDP nchini Kenya, amesema jijini Nairobi kuwa Kampeni ya “Wacha Amani Itawale” inalenga kuhimiza azma kubwa ya wadau wote kuendesha uchaguzi wa amani ili kulinda faida za maendeleo ilizopata Kenya.

Akiongea katika maadhimisho ya Kimataifa ya siku ya Kupinga matamshi ya Chuki, Mashalogu amesema kampeni hiyo pia inakusudia kuongeza ujumuishi na ushiriki wa vijana katika mchakato wa uchaguzi kwa moyo wa kutomwacha yeyote nyuma.