Mjumbe wa UM: MONUSCO kondoa wanajeshi wake katika mkoa wa Tanganyika nchini DRC inaonesha usalama umeboreka
2022-06-20 10:09:09| CRI

Naibu Mwakilishi maalumu wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Bruno Lemarquis amesema kuondolewa kwa wanajeshi wa tume ya MONUSCO katika mkoa wa Tanganyika uliopo mashariki mwa DRC ni habari njema kwani inaonesha hali ya usalama imeboreka.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa jana Jumapili, Lemarquis yupo kwenye ziara ya kikazi mkoni Tanganyika tangu Juni 7, akiwa kwenye maandalizi ya kuondolewa kwa wanajeshi wa MONUSCO mkoani hapo. Kwa mujibu wa taarifa kwa vyombo vya habari, wafanyakazi wa MONUSCO, wakiwemo wataalamu pia watabaki kwa miezi michache ili kuhakikisha mchakato wa wanajeshi hao kuondoka unafanyika bila matatizo.