Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa alaani mauaji ya raia katika eneo la Oromia nchini Ethiopia
2022-06-21 09:52:38| CRI

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Bw. Antonio Guterres amelaani mauaji ya raia yaliyotokea wikendi katika eneo la Oromia nchini Ethiopia, na kusisitiza wito wake wa kukomesha uhasama wote na wahusika wote kuhakikisha ulinzi wa raia.

Hayo yamesemwa na msemaji wake Bw. Stephane Dujarric na kuongeza kuwa katibu mkuu ameitaka serikali ya Ethiopia kuchukua hatua za haraka ili kusuluhisha mzozo wa Oromia kwa amani.

Habari zaidi zinasema kuwa maafisa wamepata miili zaidi ya 200 katika kijiji cha Tole kutokana na shambulizi la wikendi, na kulitupia lawama Jeshi la Ukombozi la Oromo kwa ukatili huo, hata hivyo jeshi hilo lilikanusha madai hayo, na kusema vikosi vya serikali ndio viliwaua raia.