TECNO yaingia upya mkataba na UNHCR ili kuongeza elimu kwa wakimbizi vijana barani Afrika
2022-06-22 09:23:31| CRI

Chapa ya simu za mkononi ya China, TECNO imetangaza kuendeleza ushirikiano wake na Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi (UNHCR) ili kuongeza upatikanaji wa elimu bora miongoni mwa vijana wakimbizi barani Afrika.

Kwa mujibu wa taarifa ya pamoja ya UNHCR na TECNO iliyotolewa mjini Nairobi, Kenya siku ya Jumanne, ili kuunga mkono Mpango wa UNHCR wa Ufadhili wa Masomo ya Wakimbizi unaojulikana kama DAFI, TECNO inataka kuhakikisha kwamba vijana waathiriwa wa mizozo barani Afrika wanapata elimu ya juu na nafasi za kazi.

Vanno Noupech, mwakilishi wa UNHCR nchini China alipongeza ushirikiano huo mpya na TECNO, akisema utahakikisha wakimbizi vijana wanatimiza ndoto zao za kitaaluma na kazi bila kukatizwa.

Ushirikiano kati ya TECNO na UNHCR ambao umekuwepo tangu mwaka 2020 umehakikisha kuwa zaidi ya watoto wakimbizi 20,000 barani Afrika wanapata elimu bora ya msingi.