Kenya yapongeza bidhaa za China zinazoendelea kupendwa
2022-06-22 09:33:26| CRI

Wakenya wamesifu bidhaa za China kama bidhaa zinazoleta mabadiliko kwenye maisha yao ya kijamii na kiuchumi.

Kuongezeka kwa umaarufu wa bidhaa za China kumetokana na kwamba bidhaa hizo zimeleta urahisi na kusaidia maisha yao. Bidhaa ambazo zinapatikana kwa wingi zaidi ni pamoja na simujanja, televisheni, spika, vyombo vya umeme vya nyumbani na jikoni pamoja na vifaa vya mahesabu.

Martin Githinji,  mwaandaaji wa maudhui ya kidigitali na mpenda teknolojia, yeye ni shabiki wa bidhaa za China kwasababu anasema zinamuwezesha kutimiza azma yake. Akiongea na mwandishi wa habari wa Xinhua wakati wa uzinduzi wa simu aina ya Tecno jijini Nairobi, Githinji amesema vitu vinavyotengezwa China vimepata watumiaji wengi nchini Kenya kwasababu wanatoa bidhaa nyingi za aina mbalimbali kwa bei tofauti.

Amebainisha kuwa kuingia kwa bidhaa za China nchini Kenya kumerahisisha kazi yake kama mwandaaji wa maudhui ya kidijitali.