Ofisa wa Uganda atoa wito wa kufanya juhudi za kuepusha msukosuko wa wakimbizi barani Afrika
2022-06-23 09:09:05| CRI

Waziri wa Mambo ya Nje wa Uganda anayeshughulikia ushirikiano wa kikanda Bw. John Mulimba ametoa wito wa kufanya juhudi za pamoja ili kuepusha msukosuko wa wakimbizi barani Afrika.

Mulimba amesema hayo alipohudhuria Mkutano wa kwanza wa Amani, Utawala Bora na Maendeleo kati ya China na nchi za Pembe ya Afrika uliofanyika tarehe 20 hadi 21 mwezi Juni mjini Addis Ababa, Ethiopia. Amesema hadi sasa Uganda imepokea wakimbizi zaidi ya milioni 1.58, na kutoa wito kwa jumuiya ya kimataifa kuunga mkono jamii za wakimbizi huko Uganda na sehemu nyingine za Afrika.

Amesisitiza kuwa nchi za Afrika zinaendelea kukabiliwa na msukosuko wa kibinadamu wenye utatanishi zaidi, hali ambayo inasababisha wakimbizi wengi wa ndani na wa nje. Hivyo ametoa wito wa kuziunga mkono kwa nguvu zote nchi na jamii zinaokumbwa na matatizo ya kibinadamu.