Wahamiaji 18 wafariki baada ya kujaribu kuingia Morocco
2022-06-27 08:44:46| cri

Wahamiaji 18 wameuawa na wengine kadhaa kujeruhiwa walipopambana na vikosi vya usalama vya Morocco walipojaribu kuingia nchini humo.

Zaidi ya wahamiaji 2,000 kutoka Kusini mwa Jangwa la Sahara walijaribu kupanda uzio wa waya kwenye mpaka wa Morocco hadi eneo la Melilla, ambapo walipambana vikali na walinzi wa mpaka wa Morocco.

Mzozo huo pia umesababisha askari 100 wa Morocco kujeruhiwa.