Bunge la Somalia lapitisha uteuzi wa Barre kuwa Waziri Mkuu wa nchi hiyo
2022-06-27 08:39:25| CRI

Bunge la Somalia limempitisha kwa kauli moja Hamza Abdi Barre kuwa waziri mkuu mpya wa nchi hiyo.

Spika wa Bunge hilo Sheikh Aden Mohamed Nur amesema, wajumbe 220 waliohudhuria kikao hicho kilichofanyika jumamosi, walimthibitisha Barre aliyeteuliwa tarehe 15 mwezi huu na rais wa Somalia Hassan Sheikh Mahamud.

Barre, ambaye alikuwepo bungeni wakati wa muswada huo, aliapishwa na kuwashukuru wabunge kwa kuwa na imani naye. Waziri Mkuu huyo mpya ana siku 30 za kuunda baraza lake jipya la mawaziri litakalokuwa na jukumu la kufanya mageuzi nchi hiyo inayokabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo usalama, ukame mkali na janga la COVID-19.