Sudan yazindua njia ya kwanza ya moja kwa moja ya majini kwenda China
2022-06-28 08:48:09| CRI

Sudan imefanya hafla ya kuzindua njia ya kwanza ya moja kwa moja ya baharini ya Sudan – China.

Waziri wa Uchukuzi wa Sudan Hisham Ali Ahmed Abuzaid na Balozi wa China nchini Sudan Ma Xinmin walikuwa miongoni mwa maofisa waliohudhuria hafla hiyo iliyofanyika mjini Khartoum jumapili jioni.

Balozi Ma amesema, Sudan, iliyoko kaskazini mashariki mwa Afrika katika pwani ya magharibi ya Bahari Nyekundu, ina fursa kubwa ya kijiografia na inatumika kama njia muhimu ya kusafirisha bidhaa za China barani Afrika tangu zama za kale.

Balozi huyo ameongeza kuwa, Sudan na China zina uwezo mkubwa wa kupanua ushirikiano wa pande hizo katika safari za baharini.