Tanzania yarejea ahadi yake ya kuhifadhi bahari na rasilimali za baharini
2022-06-28 08:47:24| CRI

Makamu wa rais wa Tanzania, Dr. Philip Mpango amerejea ahadi ya serikali ya Tanzania ya uhifadhi endelevu na matumizi ya bahari na rasilimali za baharini.

Taarifa iliyotolewa na Ofisi ya Makamu wa Rais imesema, Dr. Mpango alitoa ahadi hiyo alipohutubia Mkutano wa Umoja wa Mataifa kuhusu Bahari uliofanyika mjini Lisbon, Ureno. Dr. Mpango amesema licha ya kuridhia mapatano ya kimataifa ya kudhibiti uchafuzi baharini, Tanzania imetunga sera, mikakati na mipango ya kudhibiti uchafuzi.

Amesema Tanzania pia imechukua hatua kadhaa ikiwemo kupiga marufuku matumizi ya mifuko ya plastiki ambayo ni chanzo kikubwa cha uchafuzi katika bahari zote duniani.