Askari takriban 18 wauawa katika mapambano nchini Sudan Kusini
2022-06-28 08:49:21| CRI

Waziri wa Habari wa Jimbo la Warrap nchini Sudan Kusini Riing Deng Adiing amethibitisha kuwa, askari takriban 18 wa nchi hiyo wameuawa katika mapambano yaliyofanywa na wezi wa mifugo waliokuwa na silaha kwenye Jimbo la Warrap, kaskazini mwa nchi hiyo wikiendi iliyopita.

Deng amesema mapambano hayo yalitokea Jumapili huko Rualbet Payam baada ya askari kuwafuata vijana wenye silaha kutoka jamii ya Awan Parek ambao walikuwa waliiba ng’ombe 125 huko Aliek Payam, Kaunti ya Tonj Kaskazini.

Deng pia amesema vijana saba waliuawa kwenye mapambano hayo.