Serikali ya China yatoa shehena nyingine ya chanjo ya COVID-19 kwa Ethiopia
2022-06-28 08:45:45| cri

Hafla ya makabidhiano ya shehena nyingine ya dozi milioni 10 za chanjo ya COVID-19 zilizotolewa na serikali ya China kwa Ethiopia ilifanyika jana katika Wizara ya Afya ya Ethiopia.

Akizungumza kwenye hafla hiyo, Waziri wa Afya wa Ethiopia Bi. Lia Tadesse amesema, chanjo hizo zitaisaidia Ethiopia kupambana na janga la COVID-19 na kurejesha uchumi wake.

Naye Balozi wa China nchini Ethiopia Bw. Zhao Zhiyuan amesema chanjo hizo ni udhihirisho wa nia ya China ya kuhimiza kwa dhati ushirikiano wa kupambana na janga hilo na Afrika, na kuisaidia Ethiopia kuimarisha uwezo wake katika kupambana na janga hilo.

Hadi sasa, China imetoa dozi milioni 14 za chanjo ya COVID-19 kwa Ethiopia.