AU yatoa wito wa juhudi za pamoja kukabiliana na changamoto mbalimbali barani Afrika
2022-06-30 08:42:19| CRI

Mwenyekiti wa Kamati ya Umoja wa Afrika (AU) Moussa Faki Mahamat ametoa wito kwa nchi za Afrika kushirikiana kwa pamoja ili kukabiliana na changamoto mbalimbali zinazoathiri bara hilo.

Akizungumza kwenye kikao cha hivi karibuni cha Bunge la Afrika, Bw. Mahamat amesisitiza kuwa janga la COVID-19, mabadiliko ya tabianchi, ukosefu wa usalama na ugaidi, na mgogoro wa sasa wa chakula unaotokana na vita inayoendelea kati ya Russia na Ukraine ni miongoni mwa changamoto zinazoliathiri bara la Afrika kwa sasa.

Pia amesisitiza kuwa, hali isiyotarajiwa katika bara hilo inayohusiana na changamoto za kisiasa na kidemokrasia, zimesababisha nchi nne wanachama wa Umoja wa Afrika kusitishiwa uanachama wao.