China yazitaka pande mbalimbali zichukue hatua ili kupunguza hali ya wasiwasi nchini DRC
2022-06-30 13:31:35| cri


Naibu mjumbe wa kudumu wa China kwenye Umoja wa Mataifa Balozi Dai Bing amezitaka pande mbalimbali husika zichukue hatua kwa pamoja, ili kupunguza hali ya wasiwasi kwenye kanda ya mashariki nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC).

Balozi Dai ameyataka makundi yote yenye silaha nchini DRC yafuate pendekezo la Mchakato wa Nairobi, kusitisha shughuli zote za kimabavu, na kujiunga na mazungumzo ya kisiasa na mchakato wa kuacha silaha. Pia amesema jumuiya ya kimataifa inapaswa kuisaidia DRC kuongeza uwezo wa utawala, kuhimiza mageuzi ya idara za usalama, kutekeleza mpango wa kuacha silaha na kurudi kwenye jamii, na kulinda kihalisi ardhi na mamlaka yake.