Msaada wa chakula uliotolewa na China kwa Benin waanza kusambazwa
2022-07-01 09:50:10| cri


 

Hafla ya uzinduzi wa mradi wa msaada wa chakula uliotekelezwa kwa pamoja na serikali ya China na Shirika la Mpango wa Chakula la Umoja wa Mataifa (WFP) ilifanyika jumatano katika mji wa Adjohoun nchini Benin.

Akizungumza kwenye hafla hiyo, mwakilishi wa WFP nchini Benin amesema, mradi huo ni uungaji mkono imara wa China katika kutimiza Malengo Endelevu ya Mwaka 2030 ya Umoja wa Mataifa. Msaada huo wa tani 1,070,000 za chakula utazisaidia familia maskini elfu 100 nchini Benin, na utapunguza kwa kiasi kikubwa matatizo ya maisha kwa watu walioathiriwa na janga la COVID-19 na mafuriko.