Wauzaji wa Afrika wafikia makubaliano na waagizaji kutoka China
2022-07-01 08:44:26| CRI

Wateja 73 wa Benki ya Stanbic Bostwana ambao ni wafanyabiashara kutoka nchi 9 za Afrika wameonyesha bidhaa zao kwa zaidi ya wafanyabiashara 200 wa China waliokutana Changsha, mji mkuu wa mkoa wa Hunan nchini China na hatimaye kufikia makubaliano.

Tukio hilo limetokea jumatano wakati wa kikao cha kutangaza biashara kwa njia ya mtandao kilichoandaliwa na Benki hiyo na mbia wake, Benki ya Biashara na Viwanda ya China (ICBC), kwa ushirikiano na Maonyesho ya Uchumi na Biashara ya China na Afrika.

Mkuu wa Benki ya Stanbic nchini Botswana Philip Myburgh amesema, kwa zaidi ya muongo mmoja, Benki hiyo na mbia wake ICBC wamefanya uratibu katika kuwezesha biashara kati ya Afrika na China.