China yatoa msaada wa vifaa vya kupambana na COVID-19 kwa wakimbizi nchini Sudan Kusini
2022-07-01 08:42:35| CRI

Serikali ya China kupitia Mfuko wa Misaada wa Ushirikiano wa Kusini na Kusini (SSCAF), kwa kushirikiana na Shirika la Kuhudumia Wakimbizi la Umoja wa Mataifa (UNHCR), imetoa msaada wa zaidi ya vifaa binafsi milioni 1.3 vya kujikinga (PPE) kwa wakimbizi nchini Sudan Kusini ili kusaidia mapambano dhidi ya COVID-19.

Naibu mwakilishi wa UNHCR nchini Sudan Kusini Juliette Murekeyisoni amesema, msaada huo utasaidia kudhibiti kuenea kwa virusi vya Corona kati ya wakimbizi wanaoishi ndani na nje ya kambi zao pamoja na wenyeji wao.

Vifaa hivyo ni pamoja na glavu seti milioni 1.1, nguo za kujikinga 70,000, miwani za kujikinga 70,000 na barakoa 70,000 aina ya N95 pamoja na buti za plastiki seti 1,000.