Rais wa Misri azindua majaribio ya reli nyepesi iliyojengwa kwa ushirikiano kati ya makampuni ya China na Misri
2022-07-04 09:04:49| CRI

Rais Abdel-Fattah al-Sisi wa Misri amezindua majaribio ya reli nyepesi ya umeme iliyojengwa kwa ushirikiano kati ya makampuni ya China na Misiri, kwa kupanda treni hiyo akiwa pamoja na waziri mkuu wa Misri Bw. Mostafa Madbouly na balozi wa China nchini Misri Bw. Liao Liqiang.

Ujenzi wa mradi wa reli hiyo nyepesi ni matokeo ya mkataba wenye thamani ya dola za kimarekani bilioni 1.24 uliosainiwa baina ya Mamlaka ya ujenzi wa mahandaki ya Misri (NAT) na kundi la makampuni ya China (CREC-AVIC).

Sehemu iliyozinduliwa ina jumla ya kilometa 70 na inaunganisha eneo jipya ya makao makuu ya serikali (NAC) na miji inayozunguka eneo hilo. Waziri wa usafiri wa Misri Bw. Kamel el-Wazir amesema awamu ya kwanza itakuwa na treni 22 zitakazohudimia watu laki 3.6 kila siku.