Rais wa Zimbabwe akutana na mwanadiplomasia mwandamizi wa China kujadili uhusiano kati ya nchi zao
2022-07-04 08:53:22| CRI

Rais Emmerson Mnangagwa wa Zimbabwe jana Jumapili alikutana na mwanadiplomasia mwandamizi wa China Bw. Yang Jiechi, ambapo wamekubaliana kuimarisha mawasiliano na ushirikiano na kusukuma mbele uhusiano wa wenzi wa kimkakati wa pande zote kati ya nchi zao.

Kwenye mkutano wao uliofanyika Harare, Bw. Yang Jiechi amefikisha salamu za rais Xi Jinping wa China kwa rais wa Zimbabwe. Amesema huu ni mwaka wa 40 tangu kuanzishwa kwa uhusiano kati ya Chama cha Kikomunisti cha China CPC na Chama cha ZANU-PF cha Zimbabwe ambavyo ni vyama tawala vya nchi hizo mbili, na hali ya kuaminiana na kuungana mikono kati ya vyama hivyo viwili imeweka msingi imara wa kisiasa kwa ajili ya urafiki wa hali zote kati ya China na Zimbabwe.

Bw. Yang amesema, China inatambua nafasi muhimu ya Zimbabwe katika kuhimiza ushirikiano kati ya China na Afrika kuhusu pendekezo la "Ukanda Mmoja, Njia Moja", na iko tayari kuimarisha ushirikiano wa pande zote na Zimbabwe.