Mashirika ya China yachangia vifaa vya maji safi kwa shule kusini mwa Ethiopia
2022-07-04 09:05:33| CRI

Mashirika ya China yamechangia vifaa vya maji safi vinavyohitajika zaidi kwa baadhi ya shule zilizochaguliwa kusini mwa Ethiopia. Vifaa hivyo vimesambazwa kwenye shule mbalimbali za msingi, na vinatarajiwa kuwapatia maji safi wanafunzi 2,106 wa Ethiopia.  

Vifaa hivyo vimetengenezwa na timu ya wataalam, vikitumia nishati ya upepo kwa ajili ya pampu za kuchuja na kusafisha maji, kuendana na hali ya hewa ya Ethiopia. Licha ya changamoto zilizosababishwa na janga la Covid-19, vifaa hivyo vimefikishwa nchini Ethiopia na vimepitishwa kwenye ukaguzi na mamlaka ya chakula na dawa ya wizara ya afya ya Ethiopia.

Mke wa aliyekuwa Rais wa Ethiopia Bibi Roman Tesfaye, maofisa wa serikali za mtaa na wawakilishi waandamizi wa upande wa China walikuwepo kwenye makabidhiano ya vifaa hivyo.