Rais wa Rwanda asema mgogoro wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo unahitaji suluhisho la kisiasa
2022-07-05 08:43:59| CRI

Rais Paul Kagame wa Rwanda amesema mgogoro wa sasa na vitendo vya uhasama nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo vinahitaji utatuzi wa kisiasa na sio matumizi ya silaha.

Akiongea mjini Kigali Rais Kagame amesema Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo ina matatizo inayotakiwa kuyashughulikia kama Rwanda ilivyo na matatizo yake, lakini kisichokubalika ni kuona makundi yenye silaha kutoka nchini humo yanafanya mashambulizi na kuua watu nchini Rwanda.

Rais Kagame alikuwa anazungumza hali ya kudorora kwa uhusiano kati ya Rwanda na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, kufutia mgogoro unaoendelea unaoyahusisha makundi ya M23 FDLR na makundi mengine yenye silaha mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.