Rais Xi atoa wito wa kutanguliza maendeleo na kuweka mkazo katika ajenda ya kimataifa
2022-07-05 08:38:14| CRI

Rais Xi Jinping wa China amesema China inapenda kushirikiana na nchi mbalimbali duniani kutoa kipaumbele kwenye maendeleo na kuweka mkazo katika ajenda ya kimataifa.

Rais Xi alitoa kauli hiyo kwenye barua yake ya pongezi kwenye kongamano moja kuhusu maendeleo ya dunia lililohudhuriwa na wajumbe wa jumuiya za washauri bingwa na vyombo vya habari mjini Beijing.

Rais Xi amesema dunia ya sasa inakabiliwa na athari za mchanganiko zinazotokana na mabadiliko makubwa ya kimataifa na janga la Corona, huku ufufukaji wa uchumi wa dunia ukiwa dhaifu na pengo kati ya Kaskazini na Kusini likipanuka. Amesema wakati dunia inaingia kwenye kipindi kipya cha mtikisiko na mabadiliko, kuhimiza maendeleo kumekuwa ajenda kuu inayowakabili wanadamu, Kwa hivyo China imetoa Pendekezo la Maendeleo ya Dunia GDI.

Rais Xi amesema China iko tayari kushirikiana na nchi nyingine kufuata njia ya maendeleo inayotoa kipaumbele kwa watu, kutafuta ushirikishi na manufaa kwa wote, na kutimiza maendeleo yanayochochewa na mavumbuzi na masikilizano kati ya binadamu na mazingira ya asili.