Rais wa Msumbiji akutana na mwanadiplomasia mwandamizi wa China
2022-07-05 08:38:59| CRI

Rais Filipe Nyusi wa Msumbiji jana jumatatu alikutana na mwanadiplomasia mwandamizi wa China Bw. Yang Jiechi.

Kwenye mkutano wao uliofanyika Maputo, Bw. Yang, ambaye ni mjumbe wa Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China na mkurugenzi wa Ofisi ya Kamisheni ya Mambo ya Kigeni ya Kamati Kuu ya Chama, alifikisha salamu za rais Xi kwa rais Nyusi.

Bw. Yang amesema China itatafuta mafanikio zaidi kwenye ushirikiano kati yake na Msumbiji kwenye sekta za miundombinu, kilimo na nishati. Pia amesema China iko tayari kuendelea kuiunga mkono Msumbiji kwenye mapambano yake dhidi ya majanga ya asili na janga la Corona, na kuendeleza mawasiliano ya kitamaduni kati ya nchi mbili.