China yatoa msaada wa kinanda kikubwa kinachotembea kwa watoto wenye mahitaji maalum nchini Misri
2022-07-07 08:43:40| CRI

Ubalozi wa China nchini Misri umeipatia taasisi ya kiraia ya Mfuko wa Awldana kwa Sanaa ya Watoto wenye Mahitaji Maalum ya nchini Misri msaada wa kinanda kikubwa kinachotembea kwa ajili ya watoto wenye mahitaji maalum nchini humo.

Akizungumza na Shirika la Habari la China Xinhua, mshauri wa masuala ya kitamaduni katika Ubalozi wa China nchini Misri Yang Ronghao amesema, kinanda hicho ni tofauti na vinanda vingine, kwani kinasaidia kukuza uelewa wa sanaa kwa watoto na kuimarisha uwezo na ustadi wao wa usanii.

Ameeleza matumaini yake kuwa, shughuli kama hizo zitasaidia mawasiliano na ushirikiano kati ya watoto wa Misri na China katika maeneo mbalimbali ikiwemo sanaa, muziki na uchoraji.

Mwanzilishi na rais wa Taasisi hiyo Soheir Abdel-Kader ameeleza furaha yake kutokana na msaada huo, akisema kinanda hicho kitasaidia kuboresha vipaji vya usanii kwa watoto wenye mahitaji maalum katika Taasisi hiyo.