Shirika la Ndege la Tanzania lapanga kuanzisha safari za ndege za kwenda Windhoek, Namibia
2022-07-07 08:59:14| CRI

Shirika la Utangazaji la Namibia (NBC) limesema, nchi hiyo na Tanzania zina nia ya kufikiliana makubaliano ya kuanzisha huduma ya safari za ndege kati ya nchi hizo mbili, ambapo Shirika la Ndege la Tanzania litaanzisha safari za ndege za kwenda Windhoek, mji mkuu wa Namibia.

Akizungumza na NBC, Balozi wa Namibia nchini Tanzania Bw. Lebbius Tobias amesema Tanzania imepokea muswada husika uliowasilishwa na ujumbe wa Namibia ulioongozwa na Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi, na sasa wanafanya uthibitisho wa mwisho juu ya muswada huo.

Namibia inapanga kuitisha mkutano wa ushirikiano kati ya nchi hizo mbili mwezi Septemba mwaka huu kuzungumzia makubaliano mbalimbali yanayolenga kuendeleza uchumi wao.