Rais wa Tanzania awapa pole wanakijiji walioshambuliwa na Tembo
2022-07-07 08:34:19| CRI

Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan jana Jumatano aliwapa pole wanakijiji walioshambuliwa na Tembo na wanyama wengine wa pori.

Taarifa iliyotolewa na Ofisi ya Waziri Mkuu imesema, salamu hizo zilifikishwa na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa kwenye ziara yake katika moja ya vijiji vilivyoathirika kusini mwa Tanzania.

Bw. Majaliwa amesema, rais Samia anafahamu uharibifu wa mazao ya kilimo uliofanywa na Tembo hao, na kuwahakikishia wanakijiji hao kwamba, serikali itawapatia chakula endapo watakabiliwa na uhaba wa chakula.

Bw. Majaliwa amesema, Tembo wengi wamelazimika kukimbia maeneo ya hifadhi, ikiwemo mbuga na hifadhi za taifa, baada ya maeneo wanayoishi kuvamiwa na wafugaji.

Bw. Majaliwa amemwagiza Waziri wa Mifugo na Uvuvi Bw. Mashimba Ndaki, kukutana na wafugaji na kuwataka wasichunge mifugo yao kwenye maeneo ya hifadhi.