Umoja wa Afrika waitaka serikali ya Ethiopia kuchukua hatua za lazima kulinda usalama wa raia
2022-07-08 08:40:10| CRI

Mwenyekiti wa Kamisheni ya Umoja wa Afrika Moussa Faki Mahamat, ametoa wito kwa serikali ya Ethiopia kuchukua hatua za lazima ili kulinda usalama wa raia baada ya kurejea kwa matukio ya mauaji magharibi mwa nchi hiyo.

Kwa mujibu taarifa iliyotolewa jana Jumatano na Umoja wa Afrika, Bw. Mahamat ana wasiwasi na ripoti za mashambulizi yaliyotokea kwenye eneo la Wollega mkoani Oromia, na kusababisha vifo vya mamia ya raia.

Bw. Mahamat ameeleza kusikitishwa na vifo vya raia na kutaka uchunguzi ufanyike kuhusu mashambulizi hayo.

Kauli hizo za Bw. Mahamat zimekuja kufuatia mwendelezo wa matukio ya mauaji kwenye eneo la Wollega, ambayo serikali ya Ethiopia na manusura wamelishutumu kundi la OLA kuhusika na mashambulizi hayo.