Nchi nyingi za Afrika zaendelea na utoaji chanjo ya polio
2022-07-11 10:38:04| CRI

Ofisi ya Shirika la Afya Duniani barani Afrika imesema Malawi, Tanzania na Zambia zinatazamiwa kuanza kampeni ya awamu ya tatu ya kutoa chanjo ya polio katika wiki kadhaa zijazo, ili kukabiliana na janga la ugonjwa huo.

Tarehe 7 mwezi Julai, Msumbiji ilianza kutoa chanjo dhidi ya virusi vya polio kwa duru ya tatu.

Habari zimesema katika awamu ya kwanza na ya pili ya utoaji chanjo, Malawi, Tanzania, Zambia na Msumbiji zimepata takriban dozi milioni 36 za chanjo. Zimbabwe itashiriki kwenye awamu ya tatu na ya nne ya utoaji chanjo, ili kuhakikisha watoto wote walio chini ya umri wa miaka mitano wanapata chanjo.