Idadi ya vifo kwenye tukio la ufyatuaji risasi kwenye baa ya Johannesberg imeongezeka hadi watu 15
2022-07-11 10:34:18| CRI

Idadi ya vifo vya watu vinavyotokana na ufyatuaji risasi mapema Jumapili katika baa iliyopo Soweto huko Johannesberg imeongezeka hadi 15 baada ya mtu mwingine mmoja aliyejeruhiwa kufariki.

Akiongea na wanahabari, Mkuu wa Kitengo cha Usalama wa Jamii cha Mkoa, Faith Mazibuko, amesema inadaiwa kuwa mtu mwenye silaha alishuka kwenye teksi na kuingia kwenye baa kisha kuwafyatulia risasi watu waliomo ndani. Amesema,  hadi sasa mamlaka haijajua sababu ya washambulizi  hao kufanya tukio hilo, kwani wameingia kwenye baa wakiwa hawakuchokozwa na wala hawakuchukua pesa au kitu chochote kingine.

Awali polisi imesema kwenye taarifa kwamba, kikundi cha watu waliobeba bunduki na bastola waliingia kwenye baa saa 6:30 mchana kwa saa za huko na kuanza kuwafyatulia risasi wateja waliokuwa wamekaa ndani, ambapo  watu 12 waliuawa papo hapo kwenye eneo la tukio, na wengine 11walijeruhiwa. Watu hao wanakadiriwa kuwa na umri kati ya miaka 19 na 35. Polisi imesema inaendelea na uchunguzi juu ya tukio hilo.