Ethiopia na UM zasaini makubaliano ya kujenga upya eneo la kaskazini linalokumbwa na vita
2022-07-13 10:32:13| CRI

Wizara ya Fedha ya Ethiopia Jumanne ilitangaza kuwa imesaini makubaliano ya utekelezaji ya upande wa tatu na ofisi ya Umoja wa Mataifa inayoshughulikia mambo ya miradi (UNOPS), ili kukarabati miradi ya miundombinu katika eneo la Tigray lililoko kaskazini mwa Ethiopia.

Wizara hiyo ilitoa taarifa ikisema makubaliano hayo ni sehemu ya programu ya ukarabati wa Ethiopia unaofadhiliwa na Benki ya Dunia, ambayo inaitwa Mradi wa Ukarabati wa Jamii Zinazoathiriwa na Mapambano nchini Ethiopia.

Taarifa hiyo imesema kwa mujibu wa makubaliano na UNOPS, shirika hilo litatekeleza shughuli za kukarabati na kuboresha upatikanaji wa huduma za kimsingi na miundombinu ya jamii inayohimili hali ya hewa.