Ujenzi wa bomba la pili la kusafirisha mafuta kutoka Zambia hadi Tanzania waanza
2022-07-13 10:36:39| CRI

Waziri wa Nishati wa Zambia Bw. Peter Kapala amesema kuwa kazi za ujenzi wa bomba la pili la mafuta linalounganisha Zambia na Tanzania zimeanza kwa kujenga sehemu ya kilomita 700 katika upande wa Tanzania.

Ameongeza kuwa hivi karibuni serikali hizo mbili zimeimarisha utaratibu wa kutekeleza mfumo mzima wa mradi na bomba jipya litaanza kuingiza dizeli nchini Zambia.

Amesema katika taarifa yake kuwa upande wa Zambia uko katika hatua za mwisho za kuhitimisha utaratibu wa ufadhili wa mradi huo ambapo awamu yake ya kwanza inatarajiwa kugharimu dola za kimarekani milioni 250 na dola za kimarekani milioni 300 hadi kukamilika, ambapo gharama za jumla za mradi kwa nchi hizo mbili inakadiriwa kuwa dola za kimarekani bilioni 1.5. Amesema, mradi huo utapunguza gharama za usafirishaji na hivyo kuendelea kupunguza bei ya dizeli, ambayo kwa sasa iko juu.