Tanzania yazindua kampeni ya kuhamasisha matumizi ya nishati mbadala ili kukomesha ukataji miti
2022-07-13 10:38:21| CRI

Mamlaka nchini Tanzania zimezindua kampeni inayolenga kuhamasisha jamii kutumia nishati mbadala, ikiwa ni pamoja na kutumia gesi kupikia, ili kukomesha ukataji miti.

Waziri wa Nishati January Makamba alisema awamu ya kwanza ya kampeni hiyo itafanyika katika wilaya 38 za mikoa 14 ambapo familia maskini zinazotumia kuni kupikia zitapewa mitungi ya gesi ya kupikia bure.

Akihutubia mikutano ya hadhara katika wilaya za Butiama, Musoma na Bunda mkoani Mara wakati wa kuanza kampeni, Makamba alisema serikali itapunguza tozo za gesi ili familia masikini zimudu.

Waziri huyo aliongeza kuwa takriban watu 22,000 hufa nchini humo kila mwaka kutokana na magonjwa ya kupumua yanayosababishwa na matumizi ya kuni na mkaa.