Kamishna wa NDRMC nchini Ethiopia akamatwa kwa tuhuma za ufisadi
2022-07-14 11:09:55| CRI

Naibu kamishna wa kitengo cha uchunguzi wa uhalifu wa ufisadi cha polisi ya Ethiopia Tadesse Ayalewe jana alisema vikosi vya usalama vya nchi hiyo vimemkamata kamishna wa kamati inayoshughulikia hatari ya majanga ya Ethiopia (NDRMC) Mitiku Kassa kwa tuhuma za ufisadi.

Kwa mujibu wa habari kutoka Shirika la habari la Ethiopia (EBC) Ayalewe amesema Kassa anatuhumiwa kushirikiana na mkuu wa Shirikisho la Maendeleo na Misaada la Elshadai (ERDA) kwa kupokea na kuuza chakula na nguo za msaada kwa ajili ya “watu hewa” waliokimbia makazi kote nchini, lakini badala yake inadaiwa fedha hizo zimetumika kumnunulia nyumba kamishna huyo wa NDRMC.

Ayalewe amesema kukamatwa kwa Kassa siku ya Jumatano, kumekuja baada ya uchunguzi wa kina juu ya shughuli za mtuhumiwa. Hata hivyo polisi hawakutaja jina la mkuu wa ERDA.