Ubalozi wa China nchini Tanzania wachangia vifaa vya ofisi kwa ajili ya Kamati ya Olimpiki ya walemavu ya Tanzania
2022-07-14 11:07:43| CRI

Ubalozi wa China nchini Tanzania umechangia vifaa vya ofisi kwa ajili ya Kamati ya Olimpiki ya walemavu ya Tanzania ili kuboresha utendaji kazi wake kama kamati ambayo inaimarisha michezo kwa watu wenye ulemavu nchini humo.

Makubaliano ya mchango huo yalisainiwa na Balozi wa China nchini Tanzania Chen Mingjian na Mwenyekiti wa Kamati ya Walemavu Tuma Dandi katika Uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam. Akiushukuru ubalozi wa China, Dandi amesema mchango huo wa vifaa vya ofisi vikiwemo laptop, kompyuta za mezani, mashine ya kutolea fotokopi na projekta, umekuja kwa wakati muafaka kwani kamati hiyo inakabiliwa na changamoto nyingi zikiwemo ukosefu wa vifaa vya ofisi, hivyo vitasaidia kuboresha kazi za kamati katika kuhimiza michezo ya watu wenye ulemavu nchini humo.

Kwa upande wake balozi Chen amesema kamati hiyo imekuwa ikiunga mkono na kuhamasisha michezo kwa watu wenye ulemavu kwa miaka mingi na kuwasaidia wanariadha walemavu wa Tanzania kushiriki kwenye michezo ya walemavu ya kimataifa.