Mshauri mkuu wa mambo ya kisiasa wa China atoa wito kwa watu wa Taiwan kusimama kidete katika upande sahihi wa kihistoria
2022-07-14 12:16:01| cri

Mshauri mkuu wa mambo ya kisiasa wa China Wang Yang ametoa wito kwa watu wa Taiwan kuwa na ufahamu wa wazi wa mwelekeo wa jumla wa uhusiano wa Mlango Bahari na kusimama kidete katika upande sahihi wa kihistoria.

Wang, mjumbe wa Kamati ya Kudumu ya Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) na mwenyekiti wa Kamati ya Kitaifa ya Baraza la Mashauriano ya Kisiasa la Watu wa China, aliyasema hayo alipokuwa akihutubia mkutano mkuu wa Baraza la 14 la Mlango Bahari uliofanyika katika mji wa pwani wa Xiamen Mkoa wa Fujian mashariki mwa China.

Akinukuu barua ya rais Xi Jinping wa China ambaye pia ni katibu mkuu wa Kamati Kuu ya CPC aliyowajibu vijana kutoka Taiwan waliohudhuria kongamano hilo, Wang alisema hii inaonyesha jinsi Xi anavyowajali vijana wa Taiwan na anavyolipa umuhimu mkubwa kongamano hilo.

Wang alitoa wito kwa vijana wa pande zote mbili za Mlango Bahari kuwaunganisha vijana wengi zaidi wa Taiwan ili kutekeleza na kutimiza ndoto zao katika China bara, na kufanya maisha yao kustawi katika mchakato mkubwa wa kutimiza Ndoto ya China ya Kustawisha Taifa.