Dhana ya “Mtego wa madeni ya China” barani Afrika ni Mtego wa maneno uliotungwa na Magharibi
2022-07-15 09:30:03| CRI

Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya China Wang Wenbin amesema, “Mtego wa Madeni ya China” ni “Mtego wa Maneno” uliotungwa na nchi ambazo hazitaki kuona maendeleo ya kasi ya ushirikiano kati ya China na Afrika, na nchi nyingine zinazoendelea.

Shirika la Ufadhili la Uingereza Debt Justice hivi karibuni limetoa ripoti ikisema, madeni ya nchi za Afrika yanayotolewa na mashirika ya fedha ya watu binafsi kutoka nchi za Magharibi ni mara tatu zaidi ikilinganishwa na yale yaliyotolewa na China, na riba ni mara mbili kuliko madeni yaliyotolewa na China.
Wang Wenbin ametoa wito kwa nchi zilizoendelea na mashirika ya fedha ya watu binafsi pamoja na yale ya pande nyingine ya kimataifa, kuchukua hatua zenye ufanisi zaidi katika kutoa msaada wa fedha na kupunguza madeni kwa nchi zinazoendelea, ili kuchangia uchumi wa dunia na kutimiza maendeleo shirikishi na endelevu.