Watu wawili wauawa na wengine 15 kujeruhiwa katika shambulizi la bomu nchini Somalia
2022-07-18 08:23:01| cri

Watu wawili wameuawa na wengine zaidi ya 15 kujeruhiwa jana katika shambulizi la bomu la kujitolea mhanga lililotokea katika hoteli moja maarufu mjini Jowhar, Somalia.

Msemaji wa Mkoa wa Hirshabelle, Daud Haji alisema, huenda idadi ya vifo itaongezeka, na  aliongeza kuwa, mawaziri wawili na mbunge mmoja kutoka mkoa huo ni miongoni mwa watu waliojeruhiwa katika shambulizi hilo.

Kundi la Al-Shabab limedai kuhusika na shambulizi hilo, likisema limelenga hoteli moja yenye maafisa wa eneo la Hirshabelle.