Rwanda yazindua bustani ya burudani ya ikolojia mjini Kigali
2022-07-19 08:38:44| CRI

Serikali ya Rwanda imezindua kituo cha burudani kilichojengwa baada ya kurejeshwa kwa eneo la ardhi oevu katika mji mkuu wa nchi hiyo, Kigali.

Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Mazingira ya Rwanda Bi. Juliet Kibera amesema, bustani ya Utalii wa Ikolojia ya Nyandungu ambayo ni ya kwanza kufunguliwa mjini Kigali, inawakilisha thamani ya kurejesha mifumo ya ikolojia katika maeneo ya mijini, na itatumika kama mpango wa awali kwa maeneo mengine yenye ardhi oevu mjini Kigali na nchini humo.