Idadi ya vifo kutokana na mapigano ya kikabila nchini Sudan yaongezeka na kufikia 65
2022-07-19 08:39:42| CRI

Gazeti la Al-Sudani la Sudan limeripoti kuwa, idadi ya vifo kutokana na mapigano ya kikabila kwenye Jimbo la Blue Nile, Kusini Mashariki mwa nchi hiyo, imeongezeka na kufikia 65

Waziri wa afya wa jimbo hilo Jamal Nasir Elsayed amesema, watu 192 walijeruhiwa, na familia 120 zililazimika kukimbia makazi yao, na kwamba wengi wa waathiriwa walikuwa vijana ambao walipigwa risasi au kuchomwa visu.

Baraza la Usalama na Ulinzi la Sudan lilifanya mkutano wa dharura mjini Khartoum, ili kujadili hali ya usalama katika Jimbo la Blue Nile.

Baraza hilo limemwagiza mwanasheria mkuu wa serikali kuunda kamati ya uchunguzi na kuitaka Kamati ya usalama ya jimbo hilo kuchukua hatua za lazima za kisheria dhidi ya watu waliochochea vurugu.