Wakimbizi 2,803 warejea nchini Sudan kutoka Ethiopia
2022-07-19 09:49:44| CRI

Shirika la Kuhudumia Wakimbizi la Umoja wa Mataifa (UNHCR) limesema kwenye ripoti iliyotolewa jana, kuwa wakimbizi 2,803 wa Sudan wamerejea nchini kwao kutokea kambi ya wakimbizi nchini Ethiopia katika wiki kadhaa za karibuni.

Katika ripoti ya hali ya dharura ya Ethiopia, UNHCR ilisema wakimbizi walipitia kituo cha mpaka wa Kurmuk, katika mkoa wa magharibi wa Benishangul Gumuz.

Ripoti hiyo pia imesema, jumla ya wakimbizi 7,559 wa Sudan na  wakimbizi 452 wa Sudan Kusini wamerejea kwenye nchi zao kutoka kambi za wakimbizi nchini Ethiopia tangu mwezi Februari mwaka 2022.