Somalia yaanza uchunguzi baada ya ndege ya abiria kuanguka
2022-07-19 08:36:40| CRI

Mamlaka ya Usafiri wa Anga nchini Somalia (SCAA) imeanza uchunguzi baada ndege iliyosajiliwa nchini Kenya kuanguka katika njia ya kurukia kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Aden Adde mjini Mogadishu jana asubuhi.

Mamlaka hiyo imesema abiria wote 36 walioabiri ndege hiyo inayomilikiwa na Shirika la Ndege la Jubba waliokolewa baada ya ndege hiyo kuanguka.

Uwanja huo wa ndege wenye ulinzi mkali ni makazi ya tume za kidiplomasia, na unatumika kama kituo cha ndege za misaada ya kibinadamu nchini Somalia.