Walinda Amani nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati wafanya doria karibu 1,200 kuwasaka wapiganaji wenye silaha
2022-07-21 08:37:37| CRI

Tume ya Umoja wa Mataifa nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati (CAR) imefanya doria 1,191 katika wiki iliyopita kwa lengo kusaka makundi ya wapiganaji yenye silaha.

Naibu msemaji wa Katibu Mkuu wa Umoja huo Farhan Haq amesema jana kuwa, Tume hiyo pia iliripoti kuwa imeongeza askari wake katika eneo la Birao, wilayani Vakaga, kama hatua ya tahadhari kujibu tetesi za kutokea kwa vurugu.

Amesema mwakilishi maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja huo nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati, Valentine Rugwabiza, ametoa lita 50,000 za mafuta kwa ajili ya matumizi katika vituo vinane vya afya ili kusaidia kukabiliana na uhaba wa mafuta nchini humo.