Jengo la bunge lililojengwa kwa ufadhili wa China nchini Zimbabwe lakamilika
2022-07-21 08:36:27| CRI

Rais wa Zimbabwe Emmerson Mnangagwa ameishukuru China kwa kufadhili na kujenga jengo jipya la Bunge la nchi hiyo katika eneo la Mlima Hampden, pembezoni mwa mji mkuu wa nchi hiyo, Harare.

Akizungumza jana Jumatano katika uzinduzi wa kuweka jiwe la msingi kwa mradi mpya wa maendeleo utakaojulikana kama “Cyber City”, rais Mnangagwa amesema kumalizika kwa ujenzi wa jengo hilo kunaashiria kuanza kwa mji mpya unaotarajiwa kupunguza msongamano katika mji wa Harare.

Jengo hilo jipya la Bunge ni la kwanza la serikali kujengwa katika mji huo mpya, ambapo serikali pia inapanga kujenga majengo mengine mawili katika eneo hilo, ikiwemo jengo la Mahakama.