Uhusiano kati ya Afrika na China ni mfano mzuri wa kuigwa
2022-07-21 08:40:00| CRI

Mwenyekiti wa Kamati ya Umoja wa Afrika Moussa Faki Mahamat amesema, uhusiano kati ya Umoja wa Afrika, nchi za Afrika na China ni mfano mzuri wa kuigwa kwa zama hii.

Mahamat amesema hayo wakati akipokea barua ya uteuzi kutoka kwa Hu Changchun, kiongozi mpya wa ujumbe wa China kwenye Umoja wa Afrika huko Adds Ababa, Ethiopia. Pia ameeleza kuwa Umoja huo unapenda kuimarisha ushirikiano na China, kuharakisha utekelezaji wa makubaliano yaliyofikiwa kwenye Mkutano wa Dakar wa Baraza la Ushirikiano kati ya China na Afrika, na ujenzi wa pamoja wa “Ukanda Mmoja, Njia Moja”, ili kunufaisha zaidi watu wa Afrika na China.

Kwa upande wake, Hu amesisitiza kuwa China inaweka mkazo katika kukuza uhusiano na Umoja wa Afrika, na kupenda kuimarisha ushirikiano wa kimkakati wa kuaminiana na wa kivitendo kati ya pande hizo mbili, ili kuhimiza uhusiano kati ya China na Umoja wa Afrika ufikie kiwango kipya.